Ministry of Health

SERIKALI YAIMARISHA UWEZO WA TIMU ZA MWITIKIO WA HARAKA KUKABILIANA NA DHARURA ZA AFYA

Posted on: September 28th, 2026

Na Cletus Sanga, WAF – Mbeya

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha utayari wa kukabiliana na milipuko ya magonjwa na dharura nyingine za afya kwa kuwajengea uwezo wataalamu wanaounda Timu za Kukabiliana na Dharura za Afya (Rapid Response Teams – RRT) katika ngazi za mikoa.

Hayo yamesemwa leo tarehe 28 Septemba, 2026 na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Lucia Mkumbo, wakati wa mafunzo ya Timu za Kukabiliana na Dharura za Afya yaliyofanyika Mkoani Mbeya, ambapo amesema kuwa uwepo wa timu zenye ujuzi na uwezo wa kuchukua hatua kwa wakati ni muhimu katika kudhibiti milipuko na kupunguza madhara kwa jamii.

Dkt. Mkumbo amesema mafunzo hayo yanatoa fursa kwa wataalamu kuongeza maarifa na ujuzi wa namna ya kukabiliana na matukio ya dharura za afya, huku akisisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema, uwajibikaji na ushirikiano wa wataalamu kutoka kada mbalimbali katika kuhakikisha changamoto za kiafya zinapatiwa majibu kwa wakati.

“Mafunzo haya yanalenga kuwaongezea washiriki ujuzi wa kutekeleza majukumu yao wakati wa matukio ya dharura, ikiwemo kutambua viashiria vya awali vya mlipuko, kukusanya na kuchambua taarifa, kutoa taarifa kwa wakati, kuwasiliana kuhusu vihatarishi pamoja na kuratibu hatua za mwitikio katika ngazi ya mkoa,” amesema Dkt. Mkumbo.

Aidha, amesema mafunzo hayo yanawawezesha washiriki kujifunza kwa vitendo namna ya kufanya kazi kwa pamoja wakati wa dharura, ikiwemo kugawana majukumu, kuimarisha mawasiliano kati ya wataalamu na kuhakikisha taarifa muhimu zinawafikia wahusika kwa wakati kwa ajili ya kuchukua hatua zinazofaa.

Kwa upande wake, mtaalamu wa magonjwa ya milipuko na majanga kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Pili Kimanga, amesema mafunzo ya RRT ni muhimu katika kuongeza uwezo wa nchi wa kugundua na kuitikia kwa haraka matukio ya afya ya umma.

Amesema ushirikiano kati ya Serikali, wataalamu wa afya na wadau wa sekta mbalimbali ni muhimu katika kuimarisha mfumo wa maandalizi na mwitikio wa dharura, kwa kuwa unasaidia kuwezesha upatikanaji wa taarifa, utaalamu na utekelezaji wa hatua za pamoja pale linapoj