Ministry of Health

MKOA WA SONGWE WAENDELEA KUIMARISHA UTAYARI , KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA EBOLA NA EL NINO

Posted on: September 28th, 2026

Mkoa wa Songwe leo Septemba 28,2026 umeendelea kuchunguza maeneo na mifumo ya utayari wa kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola pamoja na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na El Nino, huku ukichukua hatua za tahadhari kutokana na nafasi yake ya kuwa mkoa wa mpakani wenye mwingiliano mkubwa wa watu.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu, Dkt. Augustino Simon amesema Songwe inakabiliwa na mazingira yanayohitaji tahadhari zaidi kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu mpakani pamoja na jiografia ya mkoa huo yenye maeneo ya milima na mabonde ambayo yanaweza kukumbwa na changamoto wakati wa mvua za El niño

Amesisitiza kuwa kutokana na hali hiyo, sekta ya afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeendelea kuchukua hatua mbalimbali, ikiwemo kubaini maeneo yenye changamoto, hususan mabondeni na milimani ambako kumekuwa na matukio ya mmomonyoko wa udongo, huku kamati ya kitaalamu yenye wataalamu mbalimbali ikiendelea kufuatilia hali na kushauri hatua stahiki.

"hatua nyingine zilizochukuliwa ni kutoa elimu kwa wananchi katika ngazi mbalimbali, kuanzia kata hadi kamati za maeneo husika, pamoja na kuhamasisha wananchi kuondoka katika maeneo yanayotambuliwa kuwa hatarishi" amesem Dkt Agustino

Aidha,ameeleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kushirikiana na jamii katika kusafisha mitaro na kuondoa taka ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua zinazotarajiwa kunyesha.

Amesema, hatua hizo zimekuja wakati timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya, ikiongozwa na Dkt. Francis Marwa, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma, ikiendelea kufanya tathmini ya utayari wa kukabiliana na Ebola na athari za El Nino katika maeneo mbalimbali kwa kutumia dodoso maalum, amesema lengo ni kubaini mapema mapungufu yaliyopo na mahitaji ya kila eneo ili hatua zinazochukuliwa ziendane na mazingira halisi.

Amesisitiza kuwa, zoezi hilo ni enedelevu na linatekelezwa na Wizara ya Afya kupitia Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu–TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu–Sera, Uratibu na Bunge, pamoja