Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 92 KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KILIMANJARO

Posted on: March 20th, 2024


Na. Majid Abdulkarim


Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi Bilioni 92 kuboresha huduma za afya mkoani Kilimanjaro.


Dkt. Mollel amebainisha hayo leo Machi 20, 2024 wakati akiwsalimia wananchi wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango aliyepo mkoani humo kwa ziara ya kikazi.


Dkt. Mollel amesema kuwa ndani kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza vifaa tiba kadha ikiwemo CT Scan kwenye hospitali ya KCMC, Mawenzi na Kibong'oto zote mkoani hapo.


Aidha amesema kuwa Rais Samia ametoa shulingi bilion 7.9 katika hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro KCMC, ambapo shulingi bilioni 5.9 ni fedha za maendeleo, zaidi ya shilingi bilion mbili za kuwezasha upatikanaji wa vifaa tiba, dawa na vitendanishi.


“Serikali ya Dkt Samia inalipa mishahara ya watumishi wote kwa asilimia 90 pale KCMC”, ameongeza Dkt. Mollel


Dkt. Mollel amefafanua kuwa, uwekezaji alioufanya Rais Samia katika sekta ya afya yeye na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu watahakikisha wanasimamia vema uwekezaji huo na kuleta tija kwa wananchi kupata Huduma bora za afya ili kuwa na taifa lenye ustawi.


MWISHO