WIZARA YA AFYA YAJIZATITI KUTOA ELIMU YA AFYA KUHUSU MPOX KATIKA MIPAKA
Posted on: August 22nd, 2024
Na. Wizara ya Afya.
Kutokana na ugonjwa wa Mpox kuripotiwa baadhi ya nchi,
Wizara ya Afya kupitia Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma imeendelea kujizatiti katika kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya Ugonjwa huo kwa kutoa vielelezo
vyenye jumbe zenye maudhui mbalimbali ya uelimishaji
kuhusu ugonjwa huo katika mipaka mbalimbali ya nchi kuanzia Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo Agust 23, 2024
Pichani ni Mkurugenzi wa Kinga Dr. Ntuli Kapologwe akiwa Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya
Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Norman Jonas leo wakitoa vielelezo vyenye jumbe zenye maudhui mbalimbali ya uelimishaji kuhusu ugonjwa wa Mpox katika kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya vielelezo hivyo ni pamoja Video pamoja vibango (Posters). Hatua hii ni utekelezaji wa maelekezo aliyotoa Waziri wa Afya Mhe Jenista Mhagama alipotembelea Kituo Jumuishi cha Forodha katika mpaka wa Namanga Mkoani Arusha wakati akikagua utayari na maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa wa Mpox usiingie nchini.
Ikumbukwe kuwa licha ya ugonjwa wa Mpox kuripotiwa baadhi ya nchi jirani lakini Tanzania bado ni salama huku hatua mbalimbali za tahadhari zikichukuliwa.