WIZARA YA AFYA, WHO WAJADILI UDHIBITI WA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KULINDA AFYA YA JAMII
Posted on: April 10th, 2026Na Happyness Hans, WAF- Morogoro
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), kupitia mpango wa kudhibiti majanga (Pandemic Fund), imeendesha kikao kazi cha mashauriano kilichowahusisha wadau kutoka sekta mbalimbali kujadili viashiria vya uchafuzi wa mazingira vinavyoweza kuathiri afya ya jamii.
Hayo yamesemwa leo Aprili 10, 2026 mkoani Morogoro na Mkuu wa Usimamizi wa Huduma za Afya Mipakani kutoka Wizara ya Afya Tanzania bara, Dkt. Remidius Kakulu wakati akifungua Kikao kazi cha wadau kuhusu ufuatiliaji wa
Viashiria vya uchafuzi katika mazingira.
Dkt. Kakulu amesema kikao hicho ni muhimu kwani kinatekeleza afua za udhibiti wa magonjwa na milipuko, ambazo zimeainishwa katika Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (National Health Security Plan) wa mwaka 2023–2029.
Ameeleza kuwa mpango huo unalenga kudhibiti magonjwa, hususan ya mlipuko, ili yasije yakasababisha madhara makubwa kwa binadamu.
Ameongeza kuwa kikao hicho cha mashauriano kimewezesha kubaini maeneo muhimu yanayopaswa kutiliwa mkazo na kuandaliwa miongozo ya kuyafuatilia, kwa lengo la kuimarisha utambuzi wa viashiria vya magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.
Kwa upande wake, Mkuu wa Usimamizi wa Huduma za Afya Mipakani kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Bi. Rukaiya Mohamed Said, amesema mkutano huo umejumuisha wadau kutoka taasisi mbalimbali zinazotekeleza udhibiti wa shughuli za kimazingira, kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, ushirikiano huo utasaidia kupata taarifa sahihi zitakazowezesha kuandaliwa kwa mwongozo wa kudhibiti vichafuzi vya mazingira, kwa lengo la kulinda afya ya jamii na mazingira.
Aidha, amesisitiza kuwa wadau wote wataendelea kushirikiana ili kuhakikisha utekelezaji wa mwongozo huo unafanikiwa na kuchangia katika kulinda afya ya jamii.
Kikao hicho kimewakutanisha wataalamu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wakiwemo wataalamu kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA), Wizara ya Maji, vitengo mbalimbali vya Wizara ya Afya, Chuo Kikuu cha Ardhi, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka ya Udhibiti