Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WANANCHI WAHAMASISHWA KUFIKA KATIKA HOSPITALI ZA WILAYA KUPATA HUDUMA ZA KIBINGWA

Posted on: June 2nd, 2025

Na. WAF, Iringa

Wananchi Mkoani Iringa wahamasishwa kufika katika katika hospitali za wilaya ili kupata huduma za kibingwa kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Dkt.Samia walioweka kambi ya siku tano (5). katika mkoa huo.

Akizungumza wakati wa kuwapokea Madaktari Bingwa na wauguzi Bingwa 34 hao leo Juni 2, 2025 kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa , Mratibu wa Ushirikiano kati ya Serikali na sekta Binafsi Dkt.Credinus Mgimba amesema anamshukuru sana Mhe.Rais Dkt.Samia kwa kupeleka huduma hizo za kibingwa ili wananchi wa Mkoa wa Iringa na maeneo jirani wanufaike bila kusafiri umbali mrefu kufuata huduma na kutumia gharama kubwa.

“ Naishukuru pia Wizara ya Afya kuendelea kuratibu zoezi hilo pamoja na wataaam hao kwa uzalendo wao wa kufika katika mkoa huo kwa ajili ya kuhudumia wananchi sambamba na kuwajengea uwezo wataoa huduma katika maeneo yao ya kazi,” amesema.Dkt. Mgimba

Naye mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Bi.Upendo Mamchony amesema awamu ya kwanza ya kambi hizo za madaktari Bingwa wa Dkt.Samia ilikuwa na mafanikio makubwa kwani wagonjwa 2566 walipata huduma za kibingwa pamoja na upasuaji kwa wagonjwa 274 wakati waliopata Rufaa ni wagonjwa 238 ambao walipona na wanaendelea vizuri na shughuli zao.

Hata hivyo mwakilishi huyo wa Wizara ya Afya amesema awamu hii wanatazamia kuhudumia zaidi ya wagonjwa 3000 mpaka 4000

Kambi hiyo ya siku tano katika mkoa wa Iringa imeanza Juni 2, 2025 na itahitimishwa Juni 6, 2025.