Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

UONGOZI MAWENZI HOSPITALI JITAZAMENI: PROF. MAKUBI

Posted on: July 9th, 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameutaka Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro kujitazama upya katika usimamizi na uwajibikaji wa utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekekezwa hospitalini hapo.

Prof. Makubi ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Julai, 2022 wakati akikagua ubora wa huduma za afya zinazotolewa kwenye jengo la kuwahudumia wagonjwa wa dharura (EMD), wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na ujenzi wa jengo la Uzazi, Mama na Mtoto.

Katibu Mkuu Prof. Makubi ameuagiza uongozi huo kukamilishwa kwa mradi wa Jengo la mama na mtoto ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.

Pro. Makubi amesema kukamilika kwa jengo hilo itasaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto wachanga, hali itakayo saidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

"Dhamira ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kuona mama mjamzito anajifungua salama na vifo vya watoto wachanga vinapungua, hivyo ubora wa huduma ndio msingi wa sekta yetu ya afya".Amesema Prof. Makubi

Akiendele na Ziara yake Prof. Makubi ameutaka uongozi wa Hospitali, wakandarasi-MCB na TAMESA kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kuhakikisha ukamlishaji wa ujenzi hauchelewi.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amesema Hospitali hiyo imeanza kupokea vifaa na wameanza kuvitumia kwenye jengo la wagonjwa wa dharura(EMD) pamoja na la wagonjwa mahututi (ICU)

Amesisitiza kuwa, kukamilika kwa ukarabati wa jengo la Wagonjwa mahututi (ICU) litaweza kuwahudumia wagonjwa mahututi wapatao 16 kwa wakati mmoja kwani vitanda 16 vimewekwa katika jengo husika.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Mawezi ni moja ya hospitali za rufaa nchini zilizopokea fedha za UVIKO-19 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo hospitalini hapo.

MWISHO