Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

TUTAPUNGUZA GHARAMA ZA KUMUONA DAKTARI - WAZIRI UMMY MWALIMU

Posted on: August 10th, 2022

Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu amesema Serikali imedhamiria kupunguza gharama za matibabu nchini Tanzania na kwakuzingatia hayo itapunguza gharama za kumuona daktari.


Waziri Ummy amesema hayo leo alipopewa nafasi ya kuzungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Wananchi katika Mkoa wa Njombe.


“Mheshimiwa Rais, kama ulivyofanya kwenye mbolea na mambo mengine, sisi pia Sekta ya Afya tumeona tunao wajibu wa kuwapunguzia mzigo Watanzania wa kulipa fedha nyingi kwa ajili ya kupata huduma katika Hospitali zetu” amesema Waziri Ummy Mwalimu


“Hivi kumuona tuu daktari unalipa 15,000 ni kwasababu gani” amehoji Waziri Ummy na kusema kuwa Timu yake ya Wizara inafanya tathmini na hivyo itashusha gharama za kumuona daktari ili kuwapunguzia mzigo Watanzania.