Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

TANZANIA, WADAU WASHIRIKIANA KUONGEZA NGUVU YA KINGA, UCHUNGUZI NA TIBA YA SARATANI

Posted on: February 4th, 2026

Na WAF, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), ikilenga kuboresha huduma za uchunguzi, matibabu na kinga ya saratani nchini.

Hayo yamebainishwa leo Februari 03, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa wakati akiupokea ujumbe wa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa IAEA katika Makao Makuu ya Wizara.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema kuwa Tanzania imefanikiwa kutekeleza jumla ya miradi 12 chini ya Mpango wa Ushirikiano wa Kiufundi wa IAEA, miradi ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uwezo wa sekta ya afya hususan katika huduma za saratani.

Kwa mujibu wa takwimu, Tanzania inakadiriwa kurekodi karibu wagonjwa wapya wa saratani 45,000 kila mwaka, huku vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vikiwa takribani 30,000. Aidha, takribani wagonjwa 27,000 sawa na asilimia 60 ya wagonjwa wapya wa saratani huhitaji huduma za tiba kwa mionzi (radiotherapy), lakini ni wagonjwa 4,000 pekee sawa na asilimia 15 wanaopata huduma hizo, hali inayoacha idadi kubwa ya wananchi bila huduma kamilifu za matibabu.

Pia, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali kwa kushirikiana na IAEA na wadau wengine imeandaa Mpango wa Taifa wa Kuharakisha Udhibiti wa Saratani (National Cancer Control Acceleration Plan) wa miaka 2023–2028, wenye thamani ya Euro milioni 90.4. Mpango huo unalenga kuongeza jitihada za kinga, uchunguzi wa mapema, upanuzi wa huduma za radiotherapy na tiba za nyuklia nchini.

Kupitia mpango huo, Serikali inalenga kuwafikia zaidi ya wananchi milioni 20 kwa ujumbe wa kinga dhidi ya saratani, wananchi milioni 1 kwa huduma za uchunguzi wa mapema, pamoja na kuongeza zaidi ya wagonjwa 10,200 watakaopata huduma za tiba kwa mionzi na tiba za nyuklia.

Amesisitiza kuwa, Mpango huo pia unakusudia kuwepo kwa huduma kamilifu za saratani katika hospitali sita za kanda ambazo ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), Kituo cha Matibabu cha KCMC, Hospitali ya Bugando, Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI),