Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

TANZANIA NA CHINA KUANZISHA MFUMO WA UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA VYA MATIBABU YA MOYO

Posted on: January 22nd, 2024

Na: WAF – Dar es Salaam

Nchi za Tanzania na China zimekubaliana kuanzisha mfumo wa wa pamoja wa upatikanaji wa vifaa tiba vinavyotumika kutoa huduma za matibabu ya moyo kutoka nchini China kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo na kutarajiwa kurahisisha upatikanaji wa vifaa vinavyotumika kutoa huduma za matibabu ya moyo na matibabu mengine yanayohitaji vifaa tiba.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mkuu kutoka Serikali ya watu wa China Mhe. Liu Guozhong Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel amesema katika majadiliano na Naibu waziri huyo China imekubali kutoa msaada wa vifaa tiba nchini pamoja na kuanza kwa ushirikiano wa kuagiza vifaa tiba nchini China.

“Tumekubaliana kupitia Bohari ya Dawa (MSD) tutaenda kushirikiana na Serikali ya Watu wa China kupata vifaa tiba ambavyo mara nyingi tumekuwa tukiviagiza katika mataifa ya mbali na kuchukua muda mrefu kutufikia”, aamesema Dkt. Mollel

Dkt. Mollel ameongezasema Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa Bohari ya Dawa (MSD) inaenda moja kwa moja katika viwanda vilivyopo nchini China kununua vifaa tiba hivyo kupunguza gharama za matibabu.

“Tanzania tayari tuna sayansi kubwa, lakini vifaa mbalimbali vinavyotumika kila siku katika kutoa huduma za matibabu havipatikani hapa nchini kwasababu hatuna viwanda vinavyozalisha vifaa hivyo”,

“Haya ni matunda ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwani tunapomuona akitembelea nchi mbalimbali duniani anafanya mambo makubwa ya ushirikiano na mataifa anayoyatembelea yaliyokuwa kisayansi na kiteknolojia ili kwapamoja tujifunze na kutumia fursa zilizopo kuendeleza sekta yetu ya afya”,ameeleza Dkt. Mollel

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge amesema JKCI imekuwa moja ya Taasisi kubwa zinazotoa huduma za matibabu ya mogonjwa ya moyo barani Afrika, na kuwa yakwanza kufanya upasuaji mkubwa wa moyo na upasuaji wa moyo kwa watoto nchini yote hayo yakiwa ni matunda ya ushirikiano wa nchi ya Tanzania na China.