Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERIKALI, WADAU WATOKOMEZA UGONJWA WA VIKOPE, HALMASHAURI 64 NCHINI

Posted on: August 4th, 2025

Na WAF, Dodoma


Serikali kwa kushirikina na Shirika la Kimataifa la Ujerumani Hellen Keller, imewatibu wagonjwa wa vikope na kutoa tiba ya upasuaji wa mtoto wa jicho kwa watu  wapatao 100,000  katika Halmashauri 64 nchini.



Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Grace Magembe ameyasema hayo Agosti 4, 2025,  mara baada ya kukutana ujumbe wa Shirika hilo katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Wizara ya Afya,Mtumba Jijini Dodoma.


 Kikao hicho kilichowakutanisha Rais wa Shirika hilo na ujumbe wake pamoja na Wizara ya Afya kilikuwa na  majadiliano yaliyolenga kuimarisha ushirikiano zaidi wa kutokomeza magonjwa yasiyoambukiza na yale  yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo afua za lishe.


Dkt. Magembe ameongeza kuwa Huduma za utoaji wa matone ya vitamini A pamoja na utoaji elimu ya masuala ya lishe hasa kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano ambao unafanyika sana mkoa wa Mara unaendelea kwa  kushirikiana na shirika la Hellen Keller.


Katika kikao hicho Wizara ya Afya imejadiliana na Shirika hilo jinsi linavyoweza kuongeza utoaji wa huduma za upasuaji wa vikope na mtoto wa jicho kwenye maeneo mengine pamoja na mafunzo kwa watumishi  wa sekta ya Afya.


“ Kama Serikali ni muhimu kuwa  na uendelevu hivyo tumekubaliana  wanapokuja na wataalam wao pia waweze kufundisha wataalam  wa ndani  ili  kuendelea kutoa huduma kama zinavyotolewa na   wataalam wa Hellen Keller  lakini pia  tumejadili namna ya kushirikiana nao kutoa elimu ya lishe  kwenye mikoa ambayo inaudumavu,” amesema Dkt. Magembe.


Naye Rais wa  Shirika la Hellen Keller Bi. Sarah Bouchie amesema shirika hilo  limefikia malengo kutokana na ushirikiano wa karibu wa Serikali na  kupongeza hatua iliyofikiwa na Tanzania  kwenye kudhibiti magonjwa hayo  na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali kutoa elimu ya masuala ya lishe  na kutokomeza  magonjwa yasiyopewa kipaumbele, lishe pamoja na yale yasiyoambukiza.