SEKTA YA AFYA YAJIPANGA KUNUFAIKA NA FURSA ZA TIBA UTALII
Posted on: February 19th, 2026Na Clement Robert, WAF – Dar es Salaam
Wizara ya afya kupitia mpango wa Tiba utalii imekutanisha wadau kutoka serikalini, sekta binafsi na taasisi mbalimbali kwa lengo la kupata maoni ili kuandaa mpango mkakati wa utalii wa matibabu
Akizungumza leo Februari 19, 2026 jijini Dar es Salaam baada ya kikao hicho Mratibu wa Tiba utalii kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita, amesema kupitia wadau hao wametazama fursa na changamoto zilizopo nchini ili kutengeneza mpango imara wa kuisaidia nchi kwenye masuala ya tiba utalii
“Tumekutana na wadau mbalimbali ili kukusanya mawazo na uzoefu wao kuhusu fursa zilizopo pamoja na changamoto tunazokutana nazo, kwa lengo la kuandaa mkakati madhubuti utakaoifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za matibabu kwa wageni kutoka nje ya nchi,” amesema Dkt. Asha Mahita.
Amesema uwepo wa agenda ya utalii wa matibabu kwenye dira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kunaongeza chachu na hamasa ya kuandaa mkakati huo kwa ubora ili kutimiza malengo ya serikali
Naye Isack Rugemarila ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya afya na magonjwa ya akili kutoka hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuandaa kikao hicho ambacho kimefungua mjadala na kuleta maoni makubwa kwenye meza moja
“Naweza nikasema huu umekuwa kama muongozo wa namna gani tunaweza kufikia lengo, na naamini hata serikali imejipanga vizuri kusimamia taasisi pia zinazotoa huduma za afya kwa watakaotoka ndani au nje ya nchi