Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MADAKTARI BINGWA WA SAMIA WAOKOA MAISHA YA MTOTO WA MIAKA SITA SIMIYU

Posted on: June 24th, 2025

Na WAF - Simiyu


Madaktari Bingwa wa Rais Samia wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kuondoa nyama za pua na mafindofindo kwenye koo (tonsils) zilizomsumbua mtoto mwenye umri wa miaka sita kwa muda  mrefu.


Akizungumzia upasuaji huo uliofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi mapema Juni 25, 2025, daktari bingwa wa upasuaji Dkt. Francis Kimwaga amesema mtoto huyo amesumbuliwa kwa muda wa miaka miwili.


Dkt. Kimwaga amesema mara ya kwanza wakati mtoto anafikishwa hospitalini hapo baada ya vipimo alishauriwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando kwani Hospitali hiyo haina uwezo na Daktari wakumfanyia upasuaji huo lakini familia ilishindwa kumudu gharama.



Kutokana na familia kushindwa kumudu gharama ilisabisha mtoto huyo kukaa na tatizo hilo kwa miaka miwili huku hali ikiendelea kuwa mbaya kila siku mpaka ujio wa Madaktari Bingwa wa Samia mkoani Simiyu ndipo amefanikiwa kufanyiwa upasuaji na kuondoa kabisa tatizo lililokua linamsumbua mtoto huyo.