Wizara Ya Afya

MAABARA YA TAIFA KUIMARISHA UDHIBITI WA MAGONJWA YA MLIPUKO

Posted on: May 20th, 2026

Wizara ya Afya kupitia Maabara ya Taifa imeendelea kuimarisha uwezo wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko kwa kutumia vifaa vya kisasa na Wataalamu wa afya. Maboresho hayo yameongeza uwezo wa uchunguzi wa haraka na ufuatiliaji wa magonjwa nchini. Serikali imeeleza itaendelea kuwekeza katika sekta ya Maabara ili kulinda afya za Wananchi.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 19 Mei, 2026 Mkoani Kilimanjaro na Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa na Afya ya Jamii, Bw. Ambele Mwafulango wakati wa ziara maalum ya kikazi yenye lengo la kuimarisha huduma za Maabara, kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchunguzi wa magonjwa na kuimarisha ushirikiano wa kitaalamu katika sekta ya afya nchini.

Amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kati ya NPHL na Taasisi za afya, tafiti na elimu ya juu, kubadilishana uzoefu, kubaini maeneo yanayohitaji maboresho pamoja na kuongeza ufanisi wa huduma za maabara nchini.

Bw. Mwafulango ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuwekeza katika ujenzi wa maabara za kisasa na ununuzi wa vifaa vya uchunguzi vyenye teknolojia ya hali ya juu ili kuongeza uwezo wa uchunguzi wa magonjwa nchini.

"Kupitia majadiliano haya ya kitaalamu, kubadilishana uzoefu na tathmini ya huduma zinazotolewa katika Taasisi mbalimbali, NPHL na wadau wake wanatafuta njia bora za kutumia teknolojia za kisasa katika uchunguzi wa magonjwa na kuongeza uwezo wa maabara zetu za ndani ili kupunguza utegemezi wa kupeleka sampuli nje ya Tanzania kwa uchunguzi zaidi ambayo itasaidia kupunguza gharama" amesema Bw.Mwafulango

Bw. Mwafulango amesema kuwa, ushirikiano kati ya Maabara ya Taifa na Taasisi za utafiti pamoja na Vyuo vya elimu ya juu ni nguzo muhimu katika kuhakikisha tafiti zinazofanyika zinatoa majibu ya changamoto halisi za afya zinazolikabili Taifa letu kwa sasa. Amebainisha kuwa kupitia ushirikiano huo, nchi itaweza kuimarisha ubunifu wa ndani katika teknolojia za uchunguzi na kuongeza kasi ya utambuzi wa magonjwa mapema.

Akihitimisha ziara hiyo Bw.Mwafulango ameeleza umuhimu wa Mafunzo endelevu kwa wataalamu wa maabara ili kuendana na