Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MAABARA JAMII YA JAMII KUTENGENEZA MKAKATI WA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MLIPUKO

Posted on: June 28th, 2025

Na WAF, Morogoro 


Wizara ya Afya kupitia Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii imeendelea kufanya

zoezi la kutengeneza mkakati wa upimaji wa magonjwa ya Mpox, Marbug na

Kipindupindu ili kuboresha huduma za upimaji wa magonjwa ya mlipuko katika Maabara za Tanzania.


Hayo yamebainishwa Juni 26, 2025 Mkoani Morogoro na Mkuu wa huduma za Maabara kutoka Wizara ya Afya Bw. Reuben Mkala wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kwa ajili ya kutengeneza mkakati wa upimaji wa magonjwa ya Mpox, Murburg na cholera "Testing strategies for priority diseases".


Bw. Mkala amesema ni wakati mzuri kwa nchi kuwa na mkakati wake ambao pale unapotokea uhitaji wa kufanya upimaji tukatumia miongozo yetu ambayo inakuwa haikinzani na miongozo ya kimataifa na pia inakuwa imezingatia uhalisia wa mazingira yetu.


“Mkakati huu utasaidia sana katika kuimarisha huduma zetu za afya hasa katika eneo la upimaji, na kutusaidia kama nchi kuweza kubaini au kuvumbua magonjwa kwa haraka kabla hayajaleta athari kubwa kwa jamii yetu, kwa sababu miongozo tayari itakuwepo na sio dharura inatokea ndio tuanze kuandaa miongozo,” amesema Bw. Mkala.


Bw. Mkala ameongeza kuwa umuhimu wa miongozo hiyo ni kuwa tayari pia ni kuepusha wataalam kuwa katika sintofahamu pindi yatokeapo magonjwa ya mlipuko.


Kwa upande wake Afisa msimamizi uboreshaji wa mifumo ya kimaabara kutoka shirika lisilo la Kiserekali la Center for International Health, Education and Biosecurity - Tanzania,(CIHEB-Tz) Bi. Adventina Chugulu amesema shirika hilo linatekeleza mradi wa USAID- Usalama wa Afya Duniani kwa kushiriana na Wizara ya Afya na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo wanajikita kwenye kuzuia, kudhibiti na kuondoa vimelea hatarishi dhidi ya magonjwa ya mlipuko.