Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA HUDUMA BORA MLOGANZILA

Posted on: February 24th, 2024



Na.WAF, Dar Es Salaam

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imeridhishwa na hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kuanzia kwa wafanyakazi, vifaa bora na vya kisasa vya kutolea huduma ambapo pia mazingira yanaridhisha na wagonjwa wanahudumiwa vizuri.

Hayo yamebainishwa leo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya ziara ya kamati ya kutembelea hospitali hiyo na kukagua maboresho ya miundombinu iliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Ndugulile amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa kujenga hospitali hiyo ambapo pia kuna kituo kingine cha utafiti wa magonjwa ya moyo ambacho kimejengwa katika eneo hilo.

“Niipongeze Serikali kwa kuboresha huduma za afya nchini kwani hivi sasa asilimia 90 ya wagonjwa ambao walikuwa wanakwenda nje ya nchi kutibiwa wanatibiwa hapa nchini na tumeanza kupata wageni kutoka nje ya nchi kuja kupata huduma nchini”. Ameeleza Dkt. Ndungulile.

Aidha, ameitaka Serikali kupanua wigo wa utoaji huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwani hospitali hiyo bado ina eneo kubwa ambapo kuna takribani ekari 3800.

"Tunahitaji upanuzi wa huduma za magonjwa ya moyo, upanuzi wa huduma za saratani, upanuzi wa huduma za magonjwa mengine ya mifupa na mfumo wa ubongo ili wananchi waweze kupata huduma bora na rahisi kwa wepesi zaidi hapa nchini". Amesema Dkt. Ndugulile.

Vile vile ameongeza kuwa kuna fedha wameambiwa zimepatikana, ujenzi unashindwa kuendelea kwa sababu ya masuala ya umiliki wa ardhi hayajakamilika hivyo kamati hiyo imeitaka Serikali kupitia Wizara ya afya na Wizara ya Elimu kukaa pamoja ili kuweza kufikia muafaka ili uwekezaji uweze kufanyika kwa sababu wananchi wanahitaji huduma bora zaidi na eneo hilo linatosha kwa matumizi yote ya elimu pamoja na huduma za afya.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye sekta ya afya hasa kwenye miundombinu, teknolojia ya afya pamoja na kwenye wataalamu, kwani kwa sasa kuna wataalamu wa kutosha