HOSPITALI BINAFSI ZAVUTIWA NA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA
Posted on: May 24th, 2024
Na WAF - Mbeya
Timu ya viongozi na wataalam wa kituo cha afya cha Mt. Theresia Wenda kutoka Iringa vijijini ikiongozwa na Mganga Mfawidhi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani Sista Dkt. Sabina Mangi, wamevutiwa na huduma za mkoba zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya.
Dkt. Mangi amesema hayo leo Mei 24, 2024 baada ya kufanya ziara ya siku moja katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa lengo la kujionea na kujifunza mambo mbalimbali ya utoaji huduma na pia kuanzisha ushirikiano na kwaajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa kituo hicho cha afya.
"Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya, imeendelea kushiriki katika kukuza na kuimarisha ubora wa huduma za afya nchini na kitovu cha huduma za afya katika Nyanda za Juu Kusini kwa kuwa na madaktari bingwa na bobezi kwa kushiriki katika utekelezaji wa huduma za kibingwa za Mkoba zinazotolewa na kambi ya Madaktari bingwa wa Dkt. Samia katika kuwahudumia wananchi." Amesema Dkt. Mangi
Aidha, Dkt. Mangi ameeleza kuwa msukumo huwo wa kuitembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya umetokanana na Madakati bingwa na bobezi kutoka hospitali ya kanda Mbeya waliokua wakitoa huduma Mkoba katika kambi ya Madaktari bingwa wa Dkt. Samia katika kituo hicho walivyokuwa wanavyofanya kazi zao kwa furaha, uadilifu kwa kufuata taalumza zao.
“Tumefika hapa tumeona kweli ni hospitali ambayo watumishi wake wanaonekana wanafuraha, wanamwamko, pamoja na hayo tumepokelewa vizuri na Mkurugenzi akatueleza siri za mafanikio hayo na jinsi wanavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na watumishi." Amesena Dkt. Mangi
Amesema, kupitia ziara hiyo wamejifunza mambo mengi ikiwemo kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano, maswala ya ubora kwa utekelezaji wa 5s KAIZEN pamoja na ushirikiano mkubwa kati ya uongozi na watumishi kwa kuishi kama familia moja.
"Dhamira yetu ni kushirikia pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya katika kuwa na huduma mkoba, pia kuanzisha programu ya kubadilishana wataalamu kwenda kituo cha afya cha Mt. Theresia na wengine kuja hapa katika Hospitali hii kwa lengo la kujengewa uwezo na kujifunza." Amesema Dkt. Mangi