Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

ELIMU YA AFYA YA UZAZI NI MUHIMU KWA VIJANA: DKT.HAONGA

Posted on: May 25th, 2024



Na WAF, Dar es Salaam

Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya Dkt. Tumaini Haonga amesema Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana ina umuhimu mkubwa kwa jamii katika kujiletea ustawi wake.

Dkt. Haonga amebainisha hayo Mei 24, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifunga Mafunzo ya Afya ya Uzazi kwa Watumishi wa Kituo cha Simu cha Wizara ya Afya( Afya Call Centre )yaliyoanza Mei 20, 2024

Dkt. Haonga ametoa wito kwa Watumishi wa Kituo cha simu cha Wizara ya Afya kuendelea kutoa ufafanuzi na elimu ya kutosha kwa vijana wanaopiga simu au watakaokutana nao wakiwa kwenye jamii , nyumbani, kwenye michezo, nyuma za ibada na mitandao ya kijamii.

“Nina imani kupitia kikao kazi hiki mtakuwa mmepata uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya afya ya uzazi kwa vijana balehe ni vema elimu mtakayoipata iwafikie na wengine"amesema Dkt. Haonga.

Dkt.Haonga afafanua kuwa ni wananchi matamarajio makubwa hususan ni kundia vijana kuwa wataweza kupatiwa taarifa sahihi zaidi kuhusiana na masuala ya afya ya Uzazi.

Ametumia nafasi hiyo kulishukuru Shirika la Elimu, Sayansi, na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa kuwezesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na wawezeshaji kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Mama na Mtoto na kuomba ushirikiano huo uwe endelevu.

Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushirikiana na UNESCO imeratibu Mafunzo ya siku tano ya Afya ya Uzazi kwa vijana hao kuanzia Mei 20-25, 2024.

MWISHO.