Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

DKT. KIKWETE KUENDELEA KUTOA MCHANGO HUDUMA ZA UZAZi, MAMA NA MTOTO

Posted on: January 24th, 2023

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete amesema huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto ni suala ambalo lipo ndani ya moyo wake na ataendelea kutoa mchango kwa Serikali na wananchi kwa ujumla.

Dkt. Kikwete ameyasema hayo wakati alipotembelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi  kwenye ofisini kwake jijini Dar ea Salaam.

Dkt. Kikwe amesema anaishukuru Serikali kupitia Wizara ya afya kwa kuendelea kumwamini na kumtumia katika mchango wake wa kuboreaha huduma katika sekta ya afya nchini.

Naye, Katibu Mkuu,Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi  ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Kiwete kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya Afya alipokiwa  Rais na baada ya kustaafu hususan katika eneo la afya ya msingi, rasilimali watu, mafunzo ya kibingwa, afya ya mama na mtoto, huduma za meno na uwekezaji mkubwa katika Hospitali ya JKCI, Mlonganzila, Benjamin Mkapa na Chuo kikuu cha  CUHAS.

Aidha, hadi sasa Rais Mstaafu anaendelea kutoa ushirikiano yeye binafsi na taasisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation kwa Wizara ya afya katika jitihada za kuboresha huduma za afya hususani  huduma za Uzazi, Mama na Mtoto na ameendelea kuwa Balozi wa jitihada za kuboresha sekta ya afya.