Wizara Ya Afya

DHAMIRA YA SERIKALI KUIMARISHA MIFUMO YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA.

Posted on: March 14th, 2026

Na Aisha Swahibu, WAF - Dodoma

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema dhamira ya Serikali ya Tanzania ni kuendelea kuimarisha usalama wa afya na utayari wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Dkt. Magembe ameyasema hayo Machi 12, 2026 wakati wa kikao kazi na ujumbe wa Shirika la International Center for AIDS Care and Treatment Programs (ICAP) uliongozwa na Mkurugenzi wa Kimataifa Dkt. Wafaa El-Sadr, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya, Mtumba jijini Dodoma, chenye lengo la kuimarisha ushirikiano uliopo katika maendeleo ya mfumo wa afya, kinga ya magonjwa, na utoaji endelevu wa huduma za afya nchini Tanzania.

Amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa, uwezo wa maabara, na mifumo ya utambuzi wa mapema ili kukabiliana kwa ufanisi na milipuko na vitisho vipya vya afya.

Aidha, Dkt. Magembe ameeleza kuwa mkakati wa taifa wa uendelevu unaolenga kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa katika mazingira ya mabadiliko ya ufadhili wa afya duniani hususan kuunganisha huduma za VVU na huduma nyingine za afya huku akiongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya uongozi na ufadhili wa sekta ya afya, pamoja na kuwaingiza taratibu watumishi wa afya waliopata mafunzo katika mfumo wa ajira wa umma.

Dkt. Magembe ametaja umuhimu unaoongezeka wa kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kupanua huduma za uchunguzi wa saratani kupitia matumizi ya teknolojia bunifu, ikiwemo afya ya kidijitali na zana za akili mnemba (AI) ambazo zinaweza kusaidia kukabiliana na uhaba wa wataalamu wa afya waliobobea.

Dkt. Magembe ameipongeza ICAP kwa kuendelea kutoa msaada wa kitaalamu na kudumisha ushirikiano na Tanzania kwa miaka mingi huku kisinia kuwa Serikali imejipanga kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya VVU na programu nyingine za afya kwa kuimarisha ujumuishaji wa huduma ndani ya mfumo wa afya wa taifa.

Kupitia Kikao hicho , Wizara ya Afya na Shirika la ICAP wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika uimarishaji wa mifumo ya maabara, kujenga uwezo wa watumishi wa afya ikiwemo eneo la tafiti