Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

BMH YAPOKEA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA

Posted on: February 9th, 2024

Na: WAF, Dodoma

Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha sekta ya afya kwa kutoa magari mawili ya kubebea wagonjwa kwa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma ili kusaidia wagonjwa wa kanda ya kati kufika kwa wakati Hospitalini.


Akizungumza baada ya hafla ya kupokea magari hayo, Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema magari hayo yataondoa changamoto ya wagonjwa wanapopata rufaa.


"Naishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha sekta ya afya na kuweka mazingira rafiki kwa wananchi kupata Huduma bora za afya”,amemshukuru Mhe. Mavunde.


Ameongeza kuwa magari ya kubebea wagonjwa ni muhimu sana kwa BMH kwani Hospitali hii imekuwa kimbilio sio tu kwa wakazi wa Dodoma na kanda ya kati bali kwa watanzania kwa ujumla.


Kwa upande wake Mkuu wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema ujio wa magari ya kubebea wagonjwa unaonyesha dhamira ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kujali afya za watanzania na kutaka taifa lenye afya bora .


"Tutasimamia magari haya yatumike kwa malengo yaliyokusudiwa ambayo ni kubeba wagonjwa ," amesisitiza Mhe. Senyamule


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Alphonce Chandika, ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuipatia Hospitali hiyo ya Kanda ya Rufaa magari hayo mawili ya kubebea wagonjwa wagonjwa.