WIZARA YA AFYA YAIMARISHA HUDUMA ZA DHARURA KUPUNGUZA VIFO VINAVYOWEZA KUZUILIKA
Posted on: November 12th, 2026Na Amos Luzuga, WAF – Arusha.
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), inaendelea kuimarisha huduma za dharura nchini kupitia mpango wa Acute Care Transformation through Basic Emergency Care (ACTxBEC).
Akizungumza leo, Novemba 12, 2026, jijini Arusha katika mkutano wa kwanza wa nchi zinazotekeleza mpango huo, Mwakilishi kutoka Kitengo cha Huduma za Dharura na Maafa cha Wizara ya Afya, Dkt. Erasto Sylivanus, amesema mpango huo unalenga kuwajengea watumishi wa afya uwezo wa kitaalamu na wa vitendo katika kukabiliana na dharura zinazotokana na ajali, matatizo ya uzazi kwa mama na mtoto, magonjwa ya kuambukiza, magonjwa ya moyo na hali nyingine zinazohatarisha maisha.
“Kuimarisha uwezo wa watoa huduma katika ngazi ya msingi ni muhimu kwa kuwa hatua za haraka na sahihi kabla ya mgonjwa kuhitaji rufaa kwenda hospitali za ngazi za juu zinaweza kuokoa maisha ya watu,” amesema Dkt. Erasto.
Hata hivyo amesisitiza kuwa takribani asilimia 50 ya vifo vinavyohusiana na hali za dharura vinaweza kuzuilika kupitia huduma bora zinazotolewa kwa wakati na hadi sasa Tanzania inalenga kuimarisha huduma hizo katika vituo 248 kwa awamu ya kwanza, hatua inayotarajiwa kuchangia kujenga taifa lenye afya bora na kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Mpango wa ACTxBEC kutoka Makao Makuu ya WHO, Profesa Teri Reynolds, amesema ushiriki wa WHO katika mkutano huo kupitia ngazi za Makao Makuu, Kanda na nchi unalenga kuimarisha utekelezaji wa mpango huo na kuhakikisha huduma bora za dharura zinawafikia wananchi katika maeneo yote
"mpango huu unalenga kuimarisha elimu, uendelevu wa huduma na kudumisha maarifa na ujuzi wa watoa huduma za afya ili kuboresha mifumo ya utoaji huduma na kukabiliana na vipaumbele vya afya vya kila nchi".amesema Dkt Teri
Mpango wa ACTxBEC ni juhudi ya kikanda inayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2026 hadi 2028 katika nchi za Tanzania, Ethiopia, Rwanda na Uganda, kwa ushirikiano wa WHO, Wizara za Afya na