Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUWA NA UJASIRI WA KITAALUMA-KAGERA

Posted on: April 10th, 2023

Na. WAF - Bukoba, Kagera

Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila amewasihi watoa huduma za afya kuwa na ujasiri wa kitaaluma wakati wote wanapokuwa wanatoa huduma za afya haswa katika magonjwa ya milipuko .

Mhe. Chalamila ametoa rai hiyo leo alipo hudhuria katika kikao maalumu kinacho fanyika kila siku katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera chenye lengo la kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya ugonjwa huo.

"Taaluma mliyoichagua ni kubwa hivyo niwaombe kuwa na ujasiri kwani msipo kuwa na ujasiri wa kitaaluma wakati wa kutoa huduma za Afya maanayake ni kuwa kazi mliyo ichagua hamja ijua vizuri" Amesema Mhe. Chalamila.

Aidha, Bw. Chalamila ameipongeza timu maalumu ya kupambana na ugonjwa wa Marburg kutoka Wizara mbalimbali pamoja na wadau wa Afya Iliopo mkoani Kagera.

Mhe. Chalamila amewashukuru na kuwapongeza watoa huduma za afya na watumishi wote kwa kazi kubwa wanayo endelea kuifanya ya kuhakikisha wanapambana na ugonjwa huu.

"Sisi katika mkoa wetu wa kagera tunawashukuru na tuna wapongeza sana kwa team work mnayofanya katika kuhakikisha tuna pambana na ugonjwa huu wa marburg maana swala hili bila nyie wataalam tusingeweza kufika hapa" Amesema Bw. Chalamila

Pia amewashukuru wadau wote wa afya kwa kuwa nao sambamba katika kipindi chote cha mapambano dhidi ya ugonjwa huo mpaka ivi sasa.

"Nawashukuru wenzetu mliopo hapa kutoka katika mashirika ya kimataifa kwa kufikisha ujumbe na taswira halisi ya nchi yetu katika mataifa mbali mbali" Amesema Mhe. Chalamila