Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

IMARISHENI MIFUMO YA TAARIFA KUDHIBITI MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Posted on: July 25th, 2024


Na WAF - Dodoma

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amewataka waratibu wa mikoa wa Magonjwa yasiyoambukiza kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa taarifa na rejesta za magonjwa kwa ajili kusaidia kufanya maamuzi sahihi.

Prof. Nagu, amesema hayo Julai 25, 2024 wakati akihitimisha kikao cha waratibu wa mikoa wa magonjwa yasiyoambukiza kilichofanyika mkoani Dodoma.

“ Nilishatoa maelekezo ya kuanzishwa kwa rejesta za magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuboresha mifumo ya ukusanyaji taarifa kwenye ngazi zote, ninafurahi kuona katika ngazi ya msingi huduma na rejesta za magojwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu imefanyiwa kazi,bado magonjwa mengine ambayo bado yanasumbua jamii, amesema Prof. Nagu na kuongeza


 "Napenda kuwakumbusha kuhusu masuala ya kuimarisha mifumo na ukusanyaji wa taarifa kwaajili ya kusaidia ukufanya maamuzi sahii kwenye maeneo yetu," amefafanua Prof. Nagu.

Mganga Mkuu huyo wa Serikali ametilia mkazo suala la ubora wa huduma kwenye magonjwa yasiyoambukiza na kupewa kipaumbele kwakua wameshuhudiwa ongezeko la watu wenye matokeo hasi ambayo yangeweza kuzuilika endapo watoa huduma wangesimamia ubora wa huduma zinazotolewa.

“Tunajukumu la kufanya kwenye kusimamia ubora wa huduma zinazotolewa, nitoe rai tukasimamie ubora wa huduma kwa kutumia vigezo sahihi, aidha nikutale Mkurugenzi wa Tiba na timu yako pamoja na Mkurugenzi wa Afya, ustawi na lishe kuhakikisha suala la ubora wa huduma linafatiliwa kwa karibu” ameagiza Prof. Nagu.

Wakati huo huo Prof. Nagu ametala jamii ipatiwe elimu sahihi ya magonjwa yasio yakuambukiza na hususani ni maeneo yenye changamoto zaidi" Amesema Prof. Nagu.

Prof. Nagu ametumia fursa hiyo kutaka ushirikiano kati ya sekta za elimu, kilimo, mazingira na ili kufikia malengo kwa haraka na ufanisi mkubwa.

Tathmini ya ubora wa huduma za MYA kwa kutumia mfumo wa ubora wa huduma za kisukari kwa kuangalia kiwango cha udhibiti wa sukari kwenye damu cha HbA1c imebainika kuwa ni asilimia 22 yaani watu 2 kati ya watu 10 ndio udhibiti wao wa sukari kwa miezi mitatu inafikia kiwango cha kuridhisha.