Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA HUDUMA ZA KIBINGWA HOSPITALI ZA MIKOA

Posted on: October 25th, 2025

Na. WAF, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe amewahimiza wananchi kutumia hospitali za Mikoa nchini kupata huduma za kibingwa, akisema Serikali imejipanga kikamilifu kuboresha huduma bora za afya katika ngazi zote.

Dkt. Shekalaghe ametoa wito huo Oktoba 24, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi ya ukaguzi shirikishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kutathmini utoaji wa huduma kwa wananchi.

Ameeleza kuwa huduma nyingi za kibingwa zinapatikana katika hospitali za mikoa, hivyo wananchi wanapaswa kuzitumia ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za Taifa, Kanda na Maalum.

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye vifaa tiba, miundombinu, dawa na watumishi. Ukipata ajali au tatizo lolote la kibingwa, unaweza kupata tiba katika hospitali ya mkoa bila kulazimika kwenda MOI au Muhimbili. Hii itapunguza muda na gharama za matibabu kwa wananchi,” amesema Dkt. Shekalaghe.

Ameendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi kufuata ushauri wa wataalam wa afya pamoja na matumizi sahihi ya dawa ili kuepuka usugu wa dawa.

Amebainisha pia kuwa Serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya ngazi zote, zikiwemo hospitali za mikoa ambazo tayari zina watumishi na miundombinu ya kutosha.
Ameitaka jamii kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha zaidi huduma katika sekta hiyo muhimu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea amesema kasi ya ukuaji wa Hospitali ya Mkoa wa Mwananyamala imekuwa kubwa katika kipindi cha miaka mitatu kutokana na ongezeko la watumishi wenye ujuzi na uboreshaji wa huduma.

“Hospitali za mikoa zimepewa jukumu la kutoa huduma za kibingwa, Mwananyamala tayari imefikisha huduma saba za kibingwa zinazotolewa, na ni kwa muda mfupi toka ipewe hadhi ya kuwa hospitali ya mkoa imekuwa ikifanya vizuri," ameeleza Dkt. Nyembea.

Ameongeza kuwa muongozo mpya wa Wizara, utaziwezesha hospitali za mikoa kuongeza huduma za kibingwa 17 ifikapo 2030 na kwa hali ilivyo, ifikapo mwaka 2030 hospitali y