WIZARA YA AFYA YAIMARISHA UTAYARI WA KUKABILIANA NA DHARURA ZA AFYA KUPITIA PHEOC
Posted on: October 15th, 2026Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na CIHEB, imefanya kikao cha kuimarisha utayari na uwezo wa kukabiliana na dharura za afya nchini kupitia Vituo vya Uratibu wa Dharura za Afya ya Umma (PHEOC), kikihusisha wataalamu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Dodoma.
Akizungumza leo Oktoba 15,2026 katika kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Dharura na Maafa, Dkt. Erasto Sylvanus, amesema kuimarisha mifumo ya afya katika ngazi zote ni muhimu katika kuhakikisha nchi inakuwa na uwezo wa kukabiliana na dharura kwa wakati.
"PHEOC si chumba chenye vifaa pekee, bali ni mfumo wa kuratibu na kusimamia mwitikio wa dharura za afya kwa ufanisi."amesema Dkt. Erasto
Hata hivyo Dkt. Erasto amesisitiza kuwa ni muhimu kupima uwezo wa wataalamu kwa vitendo kupitia mazoezi ya uigaji,kutathmini uongozi, uratibu kati ya ngazi za kit aifa na mikoa, mipango, vifaa na utayari wa watumishi ambapo hatua hiyo itasaidia kubaini mapungufu na kuhakikisha kila mhusika anaelewa wajibu wake wakati wa dharura.
Kwa upande wake, Afisa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko kutoka Shirika la Afya Duniani, Dkt. George Kauki, amesema zoezi hilo lina umuhimu katika kupima na kuimarisha uwezo wa vituo vya PHEOC vya kitaifa na mikoa, hususani wakati ambapo kuna tishio la Ebola linalohusishwa na hali ya ugonjwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kenya katika ukanda wa Afrika Mashariki.
"WHO inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuimarisha utayari na uratibu wa kukabiliana na dharura za afya."amesema Dkt Kauki
Naye Afisa Mradi kutoka CIHEB, Bw. Mololo Noah, amesema ushirikiano huo unalenga kujenga uelewa wa pamoja kuhusu taratibu za kukabiliana na dharura za afya na kubaini maeneo yanayohitaji kuimarishwa kwa ushirikiano wa wadau.
"matokeo ya zoezi hilo yatasaidia kuelekeza juhudi katika kuboresha utayari wa nchi dhidi ya magonjwa ya mlipuko, ikiwemo Ebola."amesisitiza Bw. Noah
Kuimarishwa kwa PHEOC kunalenga kuboresha mawasiliano,