Wizara Ya Afya

WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII, KUSHIRIKI KAMPENI YA BIMA YA AFYA ARUSHA

Posted on: November 11th, 2026

Na Cletus Sanga, WAF – Arusha

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini ambaye pia ni Waziri wa Hanari, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, ametoa tangazo la kuajiri Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii 154 watakaosambazwa kwenye mitaa yote ya jimbo hilo kwa lengo la kutoa elimu ya afya na kuimarisha uhusiano kati ya wananchi na vituo vya kutolea huduma.

Mhe. Makonda alibainisha hayo leo Novemba 10, 2026, wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru yaliyofanyika jijini humo ikiwa ni mpango w utatekelezaji kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri ili kusogeza huduma karibu na jamii.

Mhe. Makonda amesema wahudumu hao watakuwa kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wananchi, Ofisi ya Mbunge, zahanati, vituo vya afya, pamoja na hospitali za wilaya na mkoa, moango unatarajiwa kupunguza msongamano usio wa lazima katika hospitali kubwa kwa kutatua changamoto ndogo ngazi ya familia.

Miongoni mwa majukumu makuu ya wahudumu hao itakuwa ni kutoa elimu ya kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, kuhamasisha mtindo bora wa maisha, pamoja na kushiriki kikamilifu kampeni kubwa ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote.

Kuhusu bima hiyo, Makonda amesema Serikali imepunguza gharama ambapo sasa kiasi cha Shilingi 150,000 kinaweza kusajili familia ya watu sita kupata matibabu ya mwaka mzima.

Katika hatua nyingine, Mhe. Makonda ametangaza kuwa Jiji la Arusha linatarajia kupata uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha kuzalisha dawa za saratani pamoja na hospitali maalum ya matibabu ya ugonjwa huo, hatua inayolenga kusogeza huduma za kibingwa nchini na kuchochea utalii wa tiba kwa wageni kutoka nje.

Tayari eneo la uwekezaji huo limepatikana katika Kata ya Alternative na kuidhinishwa na Baraza la Madiwani ambapo limekabidhiwa rasmi kwa Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa ajili ya kuanza usanifu wa michoro.

Mhe. Makonda amehitimisha kwa kutoa shukrani za dhati kwa Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, pamoja na viongozi wote wa Serikali kwa ushirikiano wao mkubwa katika kusukuma mbele mipango hiyo ya maendeleo inayolenga kupunguza utege