Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WAZIRI MHAGAMA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA FALME YA LESOTHO

Posted on: April 16th, 2025

Waziri wa Afya na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jenista Mhagama amewasilisha ujumbe maalum kwa Ufalme wa Lesotho ambao umepokelewa na Waziri Mkuu wa Falme hiyo Mhe. Samuel Ntsokoane Matekane Jijini Maseru, Lesotho, Aprili 16, 2025.


Waziri Mhagama ameushukuru Ufalme wa Lesotho kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendeleza ushirikiano mzuri wa Kidiplomasia uliopo baina ya Mataifa hayo mawili.


Waziri Mhagama ameambatana na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Afrika ya Kusini, anayewakilisha  Tanzania nchini  Botswana na Falme ya Lesotho Mhe. James Bwana pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace, Magembe.