UNGA 2026: MHE.NDEJEMBI AANIKA MAFANIKIO YA RAIS SAMIA KWENYE SEKTA YA AFYA.
Posted on: September 24th, 2026Na John Mapepele, WAF- New York
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Tanzania imepunguza vifo vya akina mama kwa asilimia 80 ndani ya kipindi cha miaka saba chini ya uongozi thabiti wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Ndejembi amesema haya leo Septemba 23,2026 wakati akihutubia Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81) akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan jijini New York, Marekani.
Amefafanua kuwa dhamira ya kisiasa ni muhimu sana katika kutekeleza uwekezaji unaolenga matokeo mahususi.
Amesema uzoefu unaonesha kuwa tunapowekeza katika miradi inayotekelezeka na kuweka wananchi kuwa kiini cha mipango hiyo maendeleo yanaweza kutoka katika ahadi na kuwa matokeo yanayoweza kupimika.
"Katika hilo, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto kwa kuongeza kiwango cha wanawake wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoka asilimia 51 mwaka 2015 hadi asilimia 81 mwaka 2022" Amesema Mhe. Ndejembi.
Akiendelea kuhutubia mkutano huo Mhe. Ndejembi amesema katika misingi hiyo ambapo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alikubali jukumu la kuwa Kinara wa Afya ya Mama na Mtoto kwa Umoja wa Afrika.
Pia amesema kwa sasa dhamira ya Serikali ya Tanzania inalenga kusonga mbele katika kutekeleza ajenda ya “Three Zeros”, yaani malengo matatu ya kutokuwepo kwa vifo vya akina mama na watoto vinavyoweza kuzuilika, kutokuwepo kwa uzazi wa nyumbani, na kutokuwepo kwa watoto ambao hawajapata chanjo.
"Uzoefu wetu unaonesha kuwa hii ni ajenda ambayo Afrika inaweza kuifikia kwa mafanikio, lakini itahitaji uongozi wa kisiasa endelevu, upatikanaji wa fedha za kutosha na kuimarishwa kwa ushirikiano." ameongeza Mhe. Ndejembi
Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuungana na Tanzania katika kuipa ajenda hii msukumo mkubwa zaidi.
Awali, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) katika kikao cha 81 (UNGA Waziri wa Afya Mhe.Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza katika kikao cha ‘Sustaining Sierra Leone’s Triple Zero Gains Through 2028’, katika mjadala kuhusu namna ya kudumisha mafa