Wizara Ya Afya

TANZANIA YAJENGA MSINGI IMARA WA SERA ZA LISHE BORA NA KUDHIBITI UNENE ULIOPITILIZA NA KIRIBATUMBO

Posted on: July 14th, 2026

Na Shaban Juma, WAF – Mexico

Tanzania imeendelea kuimarisha hatua za kukabiliana na changamoto ya utapiamlo huku ikidhibiti ongezeko la unene uliopitiliza, kiribatumbo na magonjwa yasiyoambukiza yanayohusiana na lishe, hatua inayoifanya nchi kukabiliana na mzigo wa aina mbili wa matatizo ya lishe.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, wakati akishiriki kikao cha utangulizi cha Kongamano la Kimataifa kuhusu Uzito Uliozidi na Kiribatumbo (International Congress on Overweight and Obesity - ICO) linalofanyika nchini Mexico tarehe 15–17 Julai 2026 na kuandaliwa kwa ushirikiano na UNICEF.

Dkt. Magembe amesema Tanzania imefanya suala la kuzuia unene uliopitiliza kuwa sehemu ya vipaumbele vya afya ya umma, sambamba na kuendelea kupambana na changamoto ya utapiamlo, huku akieleza kuwa hatua hiyo imechangiwa na uwekezaji wa Serikali katika kuzalisha ushahidi wa kisayansi unaosaidia kufanya maamuzi ya kisera.

Amesema Tanzania imeandaa Tathmini ya Kitaifa ya Uwekezaji katika Kuzuia Uzito Uliozidi na Unene, tathmini ya ubora wa lishe wa vyakula vilivyofungashwa vinavyopatikana sokoni, pamoja na tafiti za kuelewa namna watumiaji wanavyotafsiri taarifa za lishe kwenye vifungashio vya bidhaa na jinsi zinavyoathiri maamuzi yao ya ununuzi.

Aidha, amesema Tanzania imeandaa Mfumo wa Kitaifa wa Kutathmini Ubora wa Virutubisho kwenye Vyakula (National Nutrient Profile Model) na kushiriki katika uandaaji wa Mfumo wa Pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kutathmini Ubora wa Virutubisho kwenye Vyakula, ambao utakuwa msingi wa kuandaa na kutekeleza sera mbalimbali za lishe.

Ameeleza kuwa mifumo hiyo itasaidia katika hatua za baadaye ikiwemo uwekaji wa alama za tahadhari kwenye vifungashio vya vyakula, udhibiti wa matangazo ya vyakula visivyo na afya yanayowalenga watoto, pamoja na kuboresha mazingira ya lishe katika shule na jamii.

Dkt. Magembe amesema mafanikio hayo yamewezeshwa pia na ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za utafiti, vyuo vya elimu ya juu, asasi za kiraia na washirika wa maendeleo, jambo ambalo limewezesha maamuzi ya kisera