Wizara Ya Afya

HOSPITALI YA RUFAA PWANI ITAPUNGUZA SAFARI NDEFU ZA WANANCHI KUFUATA HUDUMA

Posted on: October 4th, 2026

Na Aisha Swahibu, WAF, Pwani - Rufiji

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani utakuwa suluhisho la changamoto ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya, hususan wananchi wa Mkoa wa Pwani na maeneo jirani.

Ameyasema hayo leo Oktoba 04, 2026, mkoani Pwani, Wilaya ya Rufiji wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Chuo cha Afya cha Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Mchengerwa amesema Mkoa wa Pwani una maeneo mbalimbali, ikiwemo Wilaya ya Mafia, ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya umbali katika kupata huduma za kibingwa. Amesema ujenzi wa Hospitali hiyo utasaidia kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kupunguza muda na gharama wanazotumia kusafiri kufuata huduma.

Ameeleza kuwa, sasa baadhi ya wananchi kutoka maeneo ya Pwani hulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma katika hospitali za rufaa zilizopo mikoa mingine. Kwa baadhi ya maeneo, umbali huo ni zaidi ya kilomita 500, hali ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa wagonjwa, wazee na watu wenye mahitaji maalumu ya huduma za afya.

“Umbali huu umesababisha changamoto kwa wananchi wetu katika maeneo mbalimbali. Wananchi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya, jambo ambalo Serikali imeliona na imeamua kuchukua hatua,” amesema Mhe. Mchegerwa

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa kukamilika kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani kutanufaisha wananchi wa Pwani, wakiwemo wananchi wa Mafia, pamoja na wananchi kutoka maeneo ya jirani na mikoa mingine, kwa kuwa watapata huduma za kibingwa karibu na maeneo yao.

Mhe. Mchengerwa amebainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora bila kulazimika kusafiri umbali mrefu.

Aidha, Mhe. Mchengerwa ametoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya, akisema utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye lengo