Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

DKT. KIKWETE AKOSHWA NA HUDUMA ZA MUHIMBILI

Posted on: July 15th, 2023

Na. Mwandishi Wetu , Dar Es Salaam

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila kwa huduma nzuri wanazotoa kwa jamii na kuwataka wataalamu kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na weledi kwakuwa Watanzania wanategemea huduma wanazozitoa.

Dkt. Kikwete alitoa pongezi hizo alipotembela banda la Muhimbili Upanga na Mloganzila katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara maarufu saba saba ambapo pia amepata fursa ya kupata huduma katika banda hilo.

“Hongereni sana kwa kazi nzuri na kubwa mnayoendelea kuifanya  mkiwa kama Hospitali ya Taifa mnapaswa kuendelea kutoa huduma bora za afya nchini, alipongeza Dkt. Kikwete

Banda la Muhimbili lilikuwa linapatikana katika Ukumbi wa Kilimanjaro ambapo huduma mbalimbali zilitolewa ikiwemo huduma za Magonjwa ya Dharura, Lishe, Macho, ushauri kuhusu afya ya usikivu, vipimo vya msingi vya maabara pamoja na vipimo ya Ultrasound na ECG.