Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WADAU WAKUTANA KUJADILI MFUMO WA HUDUMA ZA AFYA KIDIGITALI WA 'AFYA SS'

Posted on: February 2nd, 2023

WIZARA ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa pamoja na wadau wake wakiwemo PATH Tanzania, wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili namna bora ya matumizi ya mfumo wa kidigitali wa Afya Supportive Supervision (AFYA SS) ilikurahisisha mfumo bora wa kisasa na kuachana na matumizi ya makaratasi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mratibu wa mafunzo hayo ya siku moja, kutoka idara ya  'Quality insurance' kitengo cha usimamizi shirikishi katika Wizara ya Afya, Dkt.Chrisogone German alibainisha kuwa, Wadau hao wameweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa lengo la kuboresha huduma bora za Afya kidigitali.


"Mfumo wa kidigitali wa supervion, ni mfumo ambao umetengenezwa kwa maana kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau mbali mbali wakiwemo PATH Tanzania kupitia mradi wao wa 'Data Use Partnership' (DUP) ili sasa tuweze kuwa na mfumo ambao utarahisisha suala la usimamizi shirikishi na kuachana na matumizi ya makaratasi. Ameeleza Dkt. Christogone German.

Aidha, amesema kuwa, wameweza kupitia masuala tofauti tofauti ya mfumo katika kuona namna bora ya kuendeleza.

"Wadau zaidi ya 30 wameweza kushiriki mkutano huu pamoja na wengine kushiriki kwa njia mtandao,

Ambapo pia wameweza kutoa maoni na namna bora ya kuendeleza mfumo huu."Alimalizia Dkt Chrisogone German.


Katika mkutano huo, Wadau hao wakiwemo Madaktari, Watalaam wa Taasisi za ndani na nje ikwemo AMREF, PATH Tanzania, Chuo Kikuu Mzumbe, TAMISEMI na wenjigine waliweza kuchangia mawazo yao katika kufanikisha maendeleo yake.