Ministry of Health

HOJA ZAIDI YA 8000 KUPITIA MFUMO WA “ONGEA NA WAZIRI” ZATATULIWA

Posted on: March 14th, 2026

Zaidi ya hoja 800 zilizowasilishwa na wananchi na watumishi wa afya kupitia mfumo wa “Ongea na Waziri” zimepatiwa majibu na hatua za utekelezaji.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Machi 13, 2026 wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, ambapo pia alishiriki katika tukio la “Ongea na Waziri” lililowakutanisha watumishi wa afya na wananchi kwa lengo la kusikiliza changamoto na kupokea maoni kuhusu utoaji wa huduma za afya.

Kupitia utaratibu huu, hoja mbalimbali zimetatuliwa kwa wakati unaofaa, ikiwemo changamoto za miundombinu, upatikanaji wa dawa, na usimamizi wa rasilimali za afya. Hii imesaidia kuimarisha imani ya wananchi na kuongeza ufanisi wa kazi kwa watumishi wa afya, ikithibitisha kuwa mfumo wa “Ongea na Waziri” ni suluhisho madhubuti la kuhakikisha kila kero inashughulikiwa kwa uwazi na kwa hara

Mfumo huu, uliozinduliwa rasmi Januari 26, 2026, unalenga kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya, na kuhakikisha kwamba maamuzi ya serikali yanaendana na mahitaji halisi ya wananchi.

Ameongeza kuwa kwa kuanzishwa kwa mfumo huu, serikali inaonyesha dhamira yake ya kutilia mkazo usikilizaji wa wananchi kama msingi wa huduma bora na uwajibikaji, hatua inayochangia moja kwa moja kuboresha sekta ya afya nchini.