Ministry of Health

TANZANIA YAKABIDHI VIFAA TIBA VYA ZAIDI YA TSH MIL. 220 KWA NCHI YA DRC KUKABILI EBOLA

Posted on: August 18th, 2026

Na Clement Robert, WAF – Dar es Salaam

Tanzania imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya takribani shilingi milioni 220 kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za nchi hiyo katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hususan Ebola.

Akizungumza leo Agosti 19, 2026 Jijini Dar es Salaam baada ya kutamatika kwa Mkutano wa Nne wa Kamati ya Uongozi ya Mawaziri wa Afya wa Ukanda wa Afrika (ReSCO), Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema msaada huo umetolewa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzingatia umuhimu wa ushirikiano wa mataifa ya Afrika katika kukabiliana na milipuko ya magonjwa

Amesema Tanzania itaendelea kuwa mshirika wa nchi nyingine pale inapohitajika sababu maradhi hayatambui mipaka ya nchi moja kwenda nchi nyingine, changamoto ya nchi moja inaweza kuwa changamoto ya nchi nyingine

“Vifaa hivi vitatumika kusaidia wahudumu wa afya walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Ebola pamoja na wananchi wanaoweza kuathirika kutokana na ugonjwa huo, na Serikali imejipanga kuhakikisha vifaa vilivyokabidhiwa vinafikishwa nchini DRC kwa wakati pindi taratibu za upokeaji zitakapokamilika” amesema Waziri mchengerwa

Aidha amesisitiza Tanzania itaendelea kuimarisha mshikamano na nchi za Afrika, akieleza kuwa hatua za pamoja na utekelezaji wa makubaliano ni muhimu zaidi katika kukabiliana na changamoto za afya ya umma kuliko maamuzi yanayobaki katika vikao pekee.

Mkutano wa ReSCO ni maandalizi ya mkutano mkuu wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika tarehe 9 – 11 Septemba 2026 Jijini Arusha ambao utawakutanisha wakuu wa nchi