Customer Feedback Centre

SHILINGI BILIONI 1.2 KUBORESHA HUDUMA ZA MACHO NCHINI

Posted on: July 23rd, 2022

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo amezindua mradi wa macho kwa Mikoa ya Tanga, Kagera, Manyara na Mtwara wenye thamani ya Tshs Bilioni 1.2 pamoja na kupokea vifaatiba vya huduma za macho vyenye thamani ya Tshs Milioni 221.5 kwa ajili ya huduma za macho kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bombo - Tanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Kilimanjaro Centre for Community Ophthalmology Tanzania(KCCO) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Bombo - Tanga, Waziri Ummy amesema vifaa tiba hivyo vitasaidia kuimarisha huduma za macho nchini.

"Huu ni mfano mzuri wa ushirikishwaji wa wadau wanaounga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha huduma za Afya hapa nchini,watanzania watanufaika na msaada huu kwa kuwa huduma za afya zinatolewa bila mipaka yeyote"

Waziri Ummy aliongeza kuwa jicho ni kiungo muhimu sana kwa binadamu hivyo basi huduma za macho zinazolenga kuzuia upungufu wa kuona na ulemavu wa kutokuona ni moja ya vipaumbele vya Sekta ya Afya.

Amesema afua zinazolenga kuboresha afya ya macho kwa jamii ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema na ustawi kwa ujumla ili kuwawezesha kushiriki kwenye shughuli za kujiletea maendeleo'ulemavu wa kutokuona unachangia kwa kiasi kikubwa kwenye umaskini wa mtu binafsi, familia na Taifa kwa ujumla'.

Hata hivyo Waziri Ummy alisema takwimu zinaonyesha kuwa watu Milioni 1 walifikiwa na huduma za macho katika vituo vya kutolea huduma za adya katika kipindi cha mwaka 2021 na kati yao 33% tayari walikuwa wana upungufu wa kuona ikijumuisha ulemavu wa kutokuona.

Aidha, 38% ya watu wenyevuhitaji wa miwani yavkurekebisha uoni walipatiwa miwani hiyo na takwimu za nchi nzima zinaonyesha kuwa watu wenye uhitaji wa huduma za macho ni takribani Milioni 12 kwa mwaka.

Vile vile aliwaasa watendaji na wasimamizi wa huduma za maxho kwenye mikoa ya Manyara, Kagera,Mtwara na Tanga wahakikishe vifaa hivyo vinatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi na vinaingizwa kwenye orodha ya vifaa vya hospitali husika na vinatunza kwa kufanyiwa matengenezo kinga ili viweze kutoa huduma kwa muda mrefu.