Customer Feedback Centre

Ministry of Health

RUFAA ZA WATOTO WACHANGA ZAPUNGUA KWA ASILIMIA 70% KATIKA HOSPITALI YA FRELIMO

Posted on: May 7th, 2024

Na WAF, Iringa

Madaktari bingwa wa Rais Samia wamesaidia katika kupunguza rufaa ya Watoto wachanga kwa zaidi ya asilimia 70 katika hospitali ya Manispaa Iringa Frelimo baada ya uanzishwaji wa wodi ya Watoto wachanga

Hayo yamebainishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Iringa (Frelimo) Dkt. Hassan Mtani wakati wa utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kutoka kwa madaktari bingwa wa Rais Samia.

Dkt. Mtani amesema madaktari wa Rais Samia wamesaidia katika kupunguza rufaa za Watoto wachanga ambapo kwa asilimia 70 ya rufaa zilizokua zinatolewa na Hospitali hiyo ni za Watoto wachanga kwakua awali hawakuweza kulaza Watoto hao kutokana na kutokua na uwezo wa kuwahudumia juu ya changamoto wanazotokana nazo.

“uwepo wa madaktari bingwa umesaidia kuanzisha vitengo mbalimbali kama vile Wodi ya matunzo ya dharura kwa Watoto wachanga (NICU), mbali ya kuwa na vifaa lakini tulikua hatuwezi namna ya kuwasaidia Watoto ambao wamezaliwa na kupata changamoto hivyo ilikua inatulazimu kuwapa rufaa lakini kwa sasa tuna ujuzi wa kuweza kuwasaidia na kupunguza rufaa za Watoto wachanga”. Amesema Dkt. Mtani.

Sambamba na hilo Dkt. Mtani amesema kuwa wamepatiwa ujuzi na kujengewa uwezo wa masuala mbalimbali ili kuweza kufanya kazi kwa weledi na kuwasaidia wananchi na ujuzi waliopatiwa kutoka kwa madaktari hao utawasaidia katika kuendelea kuboresha huduma za afya.

Hata hivyo wananchi waliojitokeza kupata huduma za madaktari bingwa wameiomba serikali kuweka utaratibu wa madaktari hao kufanya huduma hizo mara kwa mara kwani wananchi wengi wanaougua hawana gharama za kusafiri kwa ajili ya kufuata huduma za kibingwa