MAWAZIRI AFRIKA MASHARIKI WAWEKA AHADI TANO ZA KUIMARISHA, KUBORESHA AJENDA YA AFYA
Posted on: August 18th, 2026Na Clement Robert, WAF - DAR ES SALAAM.
Mawaziri wa Afya wa nchi za Afrika Mashariki wameweka ahadi tano za pamoja zinazolenga kuimarisha usalama wa afya, afya ya mama na mtoto pamoja na huduma za afya ya msingi, huku wakisisitiza umuhimu wa kubadili mikakati na maazimio kuwa utekelezaji wenye matokeo kwa wananchi.
Ahadi hizo zimewekwa wakati wa Mkutano wa Nne wa Kamati ya Uongozi ya Mawaziri wa Afya wa Kanda ya Afrika Mashariki (ReSCO) unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 18–19 Agosti 2026, ambapo Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb.), alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Mchengerwa amesema nchi za Afrika Mashariki zina wajibu wa kuhakikisha ajenda ya afya inapewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo na bajeti za kitaifa, hususan katika maeneo ya usalama wa afya, afya ya mama na mtoto na huduma za afya ya msingi.
Ahadi ya pili iliyowekwa ni kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa, maandalizi na mwitikio wa milipuko katika mipaka ya nchi ili kuwa utaratibu wa kawaida badala ya kusubiri dharura itokee. Aidha, nchi zimetakiwa kutekeleza mpango wa afya ya mama, mtoto mchanga na watoto kwa kuweka malengo ya kitaifa, muda wa utekelezaji na mifumo ya uwajibikaji.
Katika ahadi ya tatu, nchi zimeelekezwa kuimarisha utekelezaji wa mipango ya afya ya mama, mtoto mchanga na watoto kwa kuweka malengo yanayopimika, muda maalumu wa utekelezaji na uwajibikaji katika ngazi mbalimbali.
Ahadi ya nne inalenga kuongeza ufadhili wa ndani na vyanzo bunifu vya fedha za afya, sambamba na kupanua ununuzi wa pamoja wa bidhaa za afya na kuharakisha uzalishaji wa dawa, chanjo, vitendanishi na bidhaa nyingine muhimu ndani ya Afrika.
Ahadi ya tano ni kuimarisha uwajibikaji katika sekta ya afya kwa kufuatilia utekelezaji wa ahadi, kupima matokeo, kubadilishana uzoefu na kutoa taarifa za maendeleo, ili maamuzi yanayofikiwa katika ngazi ya kikanda yaonekane ka