Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MADAKTARI BINGWA WAFANYA UPASUAJI WA KUONDOA UVIMBE KG 2 NA JIWE KG 1

Posted on: June 13th, 2024


Na WAF, Kigoma


Jopo la madaktari bingwa walioweka kambi katika Hospitali ya Wilaya ya Ujiji mkoani Kigoma wamefanya upasuaji na kufanikiwa kutoa uvimbe wa kilogram 2 na jiwe la kilogram 1.2 kwa wagonjwa wawili leo, kupitia kampeni ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia.


Upasuaji huo umefanyika mapema leo Juni 13, 2024 katika Hospitali ya Halmashuri ya wilaya ya Ujiji, ambapo madaktari hao walifanya upasuaji wa kuondoa uvimbe wenye uzito wa kilogramu 2 kutoka kwa mgonjwa mmoja. Aidha, walifanya upasuaji wa kipofu kwa mgonjwa mwingine na kutoa jiwe lenye uzito wa kilogramu 1.2.


Upasuaji huo uliongozwa na Daktari bingwa wa Upasuaji Dkt. Chriss Mngere Pamoja na Dkt. Paul Myombo kwa kushirikiana na Daktari wa usingizi na ganzi Dkt. Venance John


Aidha kambi hii ni sehemu ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha ubora wa huduma za afya zinapatikana kwa Watanzania wote, hususan katika ngazi ya Halmshauri.


Madaktari hao bingwa wamekuwa wakitoa huduma Pamoja na kuwajengea uwezo watumishi katika hospitali hizo, ambapo Kampeni hii imekuwa na umuhimu mkubwa katika kuboresha afya za wananchi na kupunguza mzigo wa maradhi yanayohitaji huduma za kibingwa.