Customer Feedback Centre

Ministry of Health

KAMBI YA MADAKTARI BINGWA IENDELEE KUWEPO MARA KWA MARA ILI KIWAFIKIA WANANCHI WENGI ZAIDI

Posted on: May 7th, 2024



Na WAF-MOROGORO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali wa Mikoa na Wilaya kushirikiana kwa pamoja na kwenda kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwepo kwa Kambi za Matibabu ya Madaktari Bingwa na Ubingwa Bobezi mara kwa mara ili kuwafikia watanzania wote wenye uhitaji na matibabu ya kibingwa.

Mhe. Malima amesema hayo Mei 7, 2024 wakati akifungua kambi ya madaktari Bingwa wa Rais Samia walioweka kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Mkoani hapo.

Mhe. Malima amesema kujitokeza kwa wingi kwa Watanzania kwenye kambi ya Madaktari bingwa ni kutokana na huduma hizo zinahitajika zaidi kwa wananchi pamoja na kuwashukuru madaktari hao kwa kuwahudumia Watanzania.

“Uwepo wa madaktari hawa 56 ni jambo kubwa sana na tuko tayari kumuomba Dkt. Samia kuwepo na kambi nyingine ili kuwafikiwa Watanzania wengi zaidi, pia niwashukuru kwa kazi kubwa mnayoifanya ambapo Watanzania wamejitokeza kwa wingi, pia tunaahidi kuzidi kuwapatia ushirikiano Madaktari bingwa ili kuzidi kulifanikisha zoezi hili”. Amesema Mhe. Malima

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba Wizara ya Afya Dkt. Caroline Damian amesema hadi kufikia siku ya jana kambi zote Sita zimewahudumia wananchi zaidi ya 7,900.

“Tumshukuru Rais Samia kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika Sekta ya Afya kuanzia miundo mbinu , vifaa vya uchunguzi, ugunduzi na uwepo wa madaktari bingwa nchini ambapo wananchi wanatakiwa kuutafsiri uwekezaji huu kwa kupata huduma za kibingwa.” Amefafanua Dkt. Caroline

Naye Daktari Bingwa wa Mifupa ambae pia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi Dkt. Amani Malima amesema kambi hiyo imeweza kuwahudumia wagonjwa zaidi ya 1,500 ndani ya siku Mbili na nakuwashukuru wananchi kwa muitikio wao mkuwa wa kuja kupia afya zao.

MWISHO