Customer Feedback Centre

Ministry of Health

BIMA YA AFYA SULUJISHO LA HUDUMA BORA ZA AFYA

Posted on: July 13th, 2024

 


Na Majid Abdulkarim, KATAVI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe  Dkt Samia Suluhu Hassan  amewataka watanzania kujiunga na huduma ya Bima ya afya kwa wote ili kuzidi kuimarisha huduma za Afya nchini


Pia Mhe. Rais amewataka wananchi wa Katavi kuuza mazao ili waweze kupata fedha na  kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwa wote.


Kauli hiyo ameitoa leo Julai 13, 2024 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Serikali wakati wa kilele cha  wiki  ya Jumuiya ya Wazazi  ya Chama cha Mapinduzi kilichohitimishwa  mkoani Katavi 


Dkt Samia amesema Serikali imeendelea  kuweka misingi madhubiti ya vyanzo vya uhakika vya fedha ili kutekeleza bima ya afya kwa wote.


Amesema gharama za matibabu kwa sasa zimekuwa juu na suluhisho ni bima ya afya kwa wote.


"Niwaombe sana ndugu zangu wa Katavi unajua wakati mwingine umaskini ukiukumbatia na wenyewe unakukumbatia mnapouza mazao jitahidini kuhakikisha mnajiunga na bima ya afya kwa wote uweze unatibiwa mwaka mzima bila usumbufu" amesema Mhe. Rais na kuongeza 


"Tukifanya hivyo watanzania wote tutapata fursa ya kupata matibabu mazuri na ya viwango kulingana na uwekezaji mkubwa ulofanywanaSerikali yenu,"amesisitiza Dkt Samia.