PROF. MAKUBI AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWEZESHA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUPANDIKIZA ULOTO
Posted on: January 15th, 2026Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof. Abel Makubi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Bilioni 3 kwa ajili ya kuwawezesha watu kuweza kupata huduma za Upandikizaji wa Uloto.
Akizungumza leo Januari 14, 2026 katika kikao kazi cha Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa na watendaji wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Dodoma.
Prof. Makubi amesema Hospitali hiyo imekuwa ikitoa huduma za kibingwa na bobezi ikiwemo upandikizaji wa figo, upandikizaji wa uloto, upasuaji wa moyo na huduma nyingine za kibingwa.
"Hospitali yetu imepiga hatua kubwa katika kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa wa moyo, figo,uloto hali hii imepunguza rufaa ya wagonjwa kwenda nje ya nchi kupata matibabu", amesema Prof. Makubi.
Aidha, ameomba Waziri wa Afya, Mhe. Mchengerwa kuwaongezea watumishi wa afya wapatao 23 ili kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa watu wanaofika Hospitalini hapo kupatiwa matibabu pamoja na Vifaa vya figo na Saratani.