WIZARA YA AFYA YATWAA TUZO YA WIZARA MTAMBUKA NANE NANE 2024
Posted on: August 9th, 2024
Na WAF, DODOMA
Wizara ya Afya imetwaa Tuzo ya Wizara Mtambuka kwa kushika nafasi ya Tatu katika Maonesho Kimataifa ya Nane Nane 2024 Jijini Dodoma.
Tuzo hiyo ambayo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekabidhiwa siku moja kabla yakukamilika kwa Maonesho hayo yanayo tarajia kuhitimishwa Agosti 10, 2024.
Wizara ya Afya pamoja na Taasisi zake imekuwa moja ya Wizara Mtambuka iliyoshika nafasi za juu kwa Ubora wa Huduma ilizo zitoa kwa takribani Siku zote za maonesho, ambapo zaidi ya wananchi wasiopungua 10,000 wametembelea Mabanda ya Wizara na kupatiwa huduma.
Miongoni mwa huduma ambazo zimesha tolewa na zinaendelea kutolewa ni pamoja na Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi, Chanjo ya Homa ya Ini na Uviko-19, Elimu juu ya Afya ya Akili, Upimaji wa VVU/UKIMWI,Upimaji wa Kifua Kikuu ( TB ), Maleria pamoja na, Elimu kuhusu Tiba Asili na Elimu juu ya Lishe.