Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WAZIRI MCHENGERWA AWASILI ALGERIA, KUSHIRIKI MKUTANO WA UZALISHAJI WA DAWA, TEKNOLOJIA ZA AFYA.

Posted on: November 27th, 2025

Na WAF, Algeria

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewasili jijini Algiers, Algeria kushiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu uzalishaji wa Dawa na Teknolojia za Afya barani Afrika.

Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumedien Novemba 26, 2025, Mhe. Mchengerwa amepokelewa na Mwenyeji wake, Waziri wa Afya wa Algeria, Mhe. Muhammed Seddik Ait Messaoudene ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda vya Dawa, Mhe. Dehane Khaled. Katika mapokezi hayo pia alikuwepo Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai.

Mkutano huo utakaofanyika jijini Algiers, kuanzia Novemba 27 hadi 29, 2025 umeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria na Shirika la Afya Duniani (WHO).