Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WAAJIRI WATAKIWA KULINDA MASLAHI YA WATUMISHI WAO

Posted on: October 3rd, 2024

Na WAF- DODOMA

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko amewàgiza waajiri wote nchini kwenye sekta ya Afya kutoa ruhusa na kuwawezesha wataalam wa maabara kushiriki kwenye makongamano ya kitaaluma yanayo andaliwa na vyama vyao.

Dkt. Biteko ametoa maelekezo hayo Octoba 2, 2024 wakati akifungua Kongamano la 37 la kisayansi la wataalam wa maabara za Afya nchini na kongamano la 23 la kisayansi la Huqas na mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma

“Wataalamu wa Maabara ni watu muhimu katika kuendeleza sekta ya afya nchini, ikiwa tutawekeza kwa wataalamu hawa na kuwapatia nyenzo watakazoziitaji kutekeleza wajibu wao lakini kuhakikisha tunawatumia ibasavyo na kuwapa hadhi waataalam wa maabara nchini tutafanya tiba kuwa rahisi,” amesema Dkt. Biteko

Dkt. Biteko amewataka Wataalam wa Maabara hao kutumia fursa ya kongamano hilo kusikiliza mada zitakazotolewa, kuchangia na kujifunza ipasavyo wakati wa kongamano hilo ili maarifa hayo na uzoefu huo waweze kwenda kuwafundisha wataalamu waliopo kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya kwa watanzania.

“Nitoe wito kwenye wataalam wa. Maabara kuipenda na kuithamini taalum hii, Wanasayansi taalum yenu ni muhimu inaokoa maisha ya mwanadamu, wakati tunafanya kazi hii tukumbuke tunawahudumia watanzania walio na hali ya chini hivyo tuwahudumie kwa utu na kwa upendo”

Awali akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali chini ya Rais Wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya trioni 1.2 kuboresha miundo mbinu ya afya ikiwemo maabara za kiuchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya hali iliyochagiza wataalam wa Maabara kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Wataalam wa Maabara ni watu muhimu sana, mbali na kusomesha madaktari bingwa na bobezi basi tutaelekeza nguvu zetu pia kwa kuwasomesha wataalam wa Maabara ili tuweze kwenda sambamba na ustawi wa watanzania”

Mhe. Mhagama amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya inatambua kazi nzuri mlizofanya maboresho sheria ya Chama hiko na kuboresha huduma za maabara