Customer Feedback Centre

Ministry of Health

UTARATIBU MPYA WA UPIMAJI WA VVU KUONGEZA WIGO KWA WAPIMAJI

Posted on: July 2nd, 2024

Utaratibu mpya wa kitaifa wa upimaji wa Virusi vya UKIMWI kwa vipimo vitatu ili kuthibisha kuwa mtu ana maambukizi ya VVU utasaidia kuongeza wigo wa upimaji wa VVU nchini.


Hayo ameyasema Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini  Dkt. Ona Machangu l Julai 02, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa kikao cha kutambulisha mwongozo mpya (Algorithim) ya kitaifa kuhusu upimaji wa Virusi vya UKIMWI, ambapo mtu atapimwa ama kujipima na kugundulika kuwa na virusi vya UKIMWI kwa kipimo cha awali atalazimika kupima vipimo vingine viwili vya uhakiki ili kuthibisha kuwa anamaambukizi ya VVU.


Dkt. Machangu amesema Lengo mahususi la kutumia vipimo vitatu ni kuhakikisha wigo wa upimaji unaongezeka kwa kupima vipimo ambavyo vitaleta majibu sahihi zaidi ili kuleta manufaa na kusaidia huduma za uchunguzi kwa watu ili waweze kushawishika kupima na kuanza dozi mara moja endapo watagundulika.


Pia Dkt. Ma