Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

RC. CHACHA AAGIZA VIONGOZI WOTE TABORA KUTEKELEZA MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII.

Posted on: June 11th, 2024



Na WAF, Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Matiko Chacha amewalekeza viongozi wote ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuhakikisha kuwa wanatekeleza mpango Jumuishi wa
Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kwa mujibu wa Miongozo ya serikali.

Mhe. Chacha ametoa maelekezo hayo Juni 10,2024 wakati amefungua Kikao cha kujadili Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Mkoani Tabora.

Aidha, ametoa shukrani kwa Wadau wote wanaoendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha huduma za afya nchini.

Halikadhalika, amesisitiza kuwa kuwa katika Mkoa wa Tabora Serikali inaendekea kufanya mambo mengi katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango huu utaokuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Tabora huku akiipongeza Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI
kwa kuweka Mkoa wa Tabora miongoni mwa mikoa ya kipaumbele.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. John . Mboya amewahimiza Viongozi na wajumbe wote kuepuka vitendo vyote kinyume na mwongozo katika ngazi zote.

Wajumbe wa kikao hiki ni Viongozi mablimbali wa Mkoa na Halmashauri zote nane (8) wakiweno Wakuu wa Wikaya na Wakurugenzi