Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

RAIS SAMIA KUPOKEA TUZO YA "THE GATES GOALKEEPERS AWARD"

Posted on: February 3rd, 2025

Na WAF - Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kupokea tuzo ya “The Gates Goalkeepers Award” kama kielelezo cha matokeo makubwa ambayo yamepatikana kwenye uongozi wake kufuatia ripoti ya utafiti wa demografia na afya ya mwaka 2022 inayoonesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo Februari 3, 2025 wakati akitoa taarifa ya upokeaji wa tuzo hiyo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zinazoandaliwa na taasisi ya The Gates Foundation, mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri Mhagama amesema tukio hilo linafanyika nje ya Marekani nchini ya Tanzania kwa mara ya kwanza na Rais Samia ndiye kiongozi wa kwanza kupokea tuzo hiyo kwa bara la Afrika jambo lililochochewa na uongozi wake mahiri ulioleta mafanikio makubwa nchini hususani ni sekta ya afya kwa kuitendea haki na kusababisha mataifa makubwa duniani kutambua mchango wake.