NHIF YATAKIWA KUTOA ELIMU ZAIDI KWA JAMII KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA
Posted on: February 8th, 2024
Na. WAF, Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imeitaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuongeza ufanisi, ubunifu wa kutoa elimu juuu ya wananchi kujiunga na bima ya afya ili kuwa na wanachama wengi na mfuko kuweza kuwa endelevu
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Mhe. Stansilaus Nyongo baada ya kupokea taarifa ya hali ya utendaji na majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Mhe. Nyongo amesema kunahaja kubwa ya kusogeza elimu kwa wananchi waliopo katika ngazi ya msingi ili kuwa na uelewa na umuhimu wa bima ya afya kabla ya kuanza kutekeleza sheria ya bima yafya kwa wote.
“Naimani kubwa mkifanikiwa katika kutoa elimu kwa jamii ya ngazi ya msingi sheria ya bima ya afya kwa wote ikianza kutekelezwa wananchi watakuwa tayari wanauelewa juu ya kuwa na bima ya afya”, amesisitiza Mhe. Nyongo
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile ametoa wito kwa uiongozi wa NHIF pamoja na wizara kufanya tafiti mbalimbali juu ya uendeshaji wa mfuko wa taifa wa bima ya afya ili kupata ujuzi namna ya kuendesha mfuko huo wakati sheria ya bima yafaya kwa wote itakapo anza kutumika