MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WAZINDUA JENGO LA UPASUAJI MONDULI
Posted on: October 25th, 2024
Na WAF - MONDULI
Timu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia iliyoweka kambi wilayani Monduli mkoani Arusha imefanikiwa kuzindua jengo jipya la upasuaji katika Hospitali ya wilaya ikiwa ni muendelezo wa kambi ya kibingwa awamu ya pili Wilayani humo.
Akizungumza Hospitalini hapo Muuguzi Mfawidhi Anna Manga amesema jengo walilokuwa wakilitumia lilikuwa la muda mrefu na hata miundombinu yake ya maji na umeme ilikuwa chakavu.
"Tangu kujengwa kwa jengo hili jipya lilikuwa halijaanza kufanya kazi hivyo walipokuja mabingwa hawa wa Rais Samia tukasema tutumie fursa hii kuanza upasuaji kwani hata vifaa vyake ni vipya na vilihitaji utaalam kidogo," amesema Muuguzi Manga.
Akizungumza hospitalini hapo Daktari Bingwa wa usingizi na ganzi salama Dkt. Moa Kalunga kutoka Mloganzila amesema ipo haja ya hospitali zilizopo ngazi ya msingi kuongezewa nguvu ili ziweze kutoa huduma zenye tija kwa wananchi.
"Ukifika huku ndio utajua wananchi wanahitaji huduma, mbali ya kwamba jamii hii ni ya wafugaji lakini muamko wakwemda kuwaona wataalam kwenye vituo vya afya ni mkubwa," amesema Dkt. Kalunga.
Akiongea na Mganga Mkuu wa wilaya mara baada ya kutembelea Hospitalini hapo na kuona huduma za kibingwa Katibu wa Afya kutoka Wizara ya Afya Rahim Ngaweji amewaasa wananchi wilaya humo kuendelea kujitokeza.
"Kambi yetu ya Madaktari Bingwa itaendelea hadi tarehe 26 siku ya jumamosi, niendelee kuwaomba wananchi kujitokeza kwa siku hizi tatu zilizosalia kwa ajili ya kujipatia huduma za Kibingwa na Bobezi.